Al-Baqara
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَٱسْتَبِقُوا۟ ٱلْخَيْرَٰتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا۟ يَأْتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ 148
(148) Yani kila watu wa dini fulani na mila fulani wana mwelekeo wanaouelekea katika ibada zao. Na jambo la muhimu si katika kukielekea kibla. Kwa sababu, ni miongoni mwa sheria ambazo hubadilishwa na nyakati na hali, na zinaingiwa na ufutaji na kugeuzwa kutoka upande mmoja hadi upande mwingine. Lakini, jambo lote kabisa ni katika kutekeleza utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake na kutafuta ukaribu mno naye. Hiki ndicho kichwa cha furaha na hati ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Nacho ndicho ikiwa nafsi hazitasifika kwacho, basi zitapata hasara ya duniani na Akhera. Kama vile ikiwa (nafsi) zitasifika kwacho, basi hizo ndizo zenye faida kwa hakika. Na hili ni jambo lililokubaliwa katika sheria zote. Nalo ndilo ambalo Mwenyezi Mungu aliumba viumbe kwa ajili yake, na akawaamrisha kulifanya. Na amri ya kushindana kuendea mema ni kiwango cha ziada juu ya amri ya kutenda mema tu. Kwani, kushindana kuyaendea (mema), kunajumuisha kuyafanya, kuyakamilisha, na kuyatekeleza katika hali bora zaidi, na kuyakimbilia. Na mwenye kushindana katika heri duniani, basi yeye ndiye wa kwanza Akhera kwenda Peponi. Kwa hivyo, wanaoshindana ndio wa daraja la juu kabisa miongoni mwa viumbe. Nazo heri zinajumuisha mambo ya faradhi yote na ya sunna kama vile Swala, Swaumu, Zaka, Hija, 'Umra, Jihad, na manufaa yanayowafikia wengine; na yale yasiyowafikia wengine. Na kwa kuwa jambo lenye nguvu zaidi linalozihimiza nafsi kukimbilia heri na kuzitia nguvu ni yale aliyoyawekea Mwenyezi Mungu ya malipo, akasema: “Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” Atawakusanya Siku ya Kiyama kwa uwezo wake, na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake, “ili awalipe waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na awalipe waliotenda mema kwa wema.” Na Aya hii tukufu inatumiwa kama ushahidi wa kufanya kila jema ambalo matendo yanasifika kwalo, kama vile kuswali mwanzoni mwa wakati wake, kuharakisha kutekeleza faradhi za kufunga, Hija na 'Umra, na kutoa Zaka, na kutekeleza sunna za ibada na adabu zake. Basi ee Mwenyezi Mungu! Ni ya kujumuisha na kunufaisha kulikoje huku kwa Aya hii!