سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
سورت 18

Al-Kahf

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 31

أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ جَنَّـٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمُ ٱلْأَنْهَـٰرُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ ۚ نِعْمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا 31

{31} Na akataja malipo yao kwa kauli yake, "Hao watapata Bustani za milele, zinazopita mito kwa chini yao. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na atilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi." [Hao] yaani, wale waliosifiwa kwa Imani na matendo mema, wana bustani za juu ambazo miti yake ni mingi, kwa hivyo ikawasitiri waliomo humo, na mito yake ikawa mingi, kwa hivyo ikawa inapita kwa chini yake miti hiyo ya maridadi, na majumba ya kifahari. Na mapambo yao humo ni dhahabu, na mavazi yao humo ni hariri ya kijani kibichi kutoka kwa hariri nzito. Watakuwa wameegemea humo juu ya makochi. Navyo ni vitanda vilivyopambwa na kurembeshwa kwa nguo za kifahari. Na kuegemea kwao kwenye makochi hayo kunaonyesha kupumzika kwao kamili, na kutokuwa kwao na uchovu na tabu, na pia kuhudumiwa kwao na watumishi kwa chochote wanachotamani, na utimilifu wa hayo yote ni kudumu na kukaa humo milele. Na nyumba hii tukufu ndiyo, "malipo bora zaidi!" kwa watendao matendo. "Na ndiyo matandiko mazuri mno ya kupumzikia." Watapumzikia hapo na kujistarehesha kwa yaliyomo ndani yake miongoni mwa yale yanayotamaniwa na nafsi, na kupendeza macho miongoni mwa furaha na raha ya daima, na matamu ya mara kwa mara, na neema na baraka nyingi. Na ni mapumzikio gani ambapo ni pazuri zaidi kuliko nyumba ambayo wa chini zaidi kati ya wakazi wake anatembea katika ufalme wake, na neema zake, na makasri yake, na bustani zake kwa muda wa miaka elfu mbili? Naye haoni kwamba kuna neema yoyote zaidi ya ile aliyo ndani yake. Amepewa matamanio yake na matakwa yake yote, na hata akazidishiwa katika matakwa yake yale ambayo matamanio yake hayakuweza kuyafikia. Na licha ya hayo, furaha yao hiyo ni ya kudumu na kuzidi katika sifa zake na uzuri wake. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mkarimu asitunyime heri aliyo nayo kwa sababu ya uovu tulio nao unaotokana na kutotekeleza kwetu mambo vyema na uasi wake. Na Aya hii tukufu na Aya zinazofanana nayo ziliashiria kuwa mapambo hayo yanawajumuisha wanaume na wanawake, kama ilivyokuja katika riwaya zilizo sahihi, kwa sababu aliliwacha katika hali ya ujumla katika kauli yake, "watapambwa", na kadhalika hariri na mengineyo.