سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
سورت 16

An-Nahl

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 90

إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ وَٱلْإِحْسَـٰنِ وَإِيتَآئِ ذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ ٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ وَٱلْبَغْىِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ 90

{90} Na uadilifu ambao Mwenyezi Mungu aliamuru unajumuisha kufanya uadilifu katika haki yake na haki ya waja wake. Basi uadilifu katika hayo ni kutekeleza haki mbalimbali kikamilifu na kwa wingi. Kwamba mja atekeleze kile ambacho Mwenyezi Mungu alimuwajibishia miongoni mwa haki za kimali na za kimwili na zenye kuchanganya mbili hizo katika haki zake Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na kwamba aamiliane na viumbe kwa uadilifu kamili. Kwa hivyo akatekeleza kila mlezi kile kilicho juu yake chini ya ulezi wake, sawa iwe ni katika usimamizi na uongozi mkuu, na usimamizi wa kutoa hukumu, na makamu wa kiongozi mkuu, na makamu wa mahakimu. Na uadilifu ni kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwafaradhishia katika Kitabu chake na juu ya ulimi wa Mtume wake na akawaamuru kuifuata. Na uadilifu katika miamala ni kutimiza yote yanayokulazimu katika mikataba ya kuuza, kununua, na mabadilishano mengineyo. Kwa hivyo haufai kuwapunja haki yoyote katika hayo, wala kuwadanganya, wala kuwahadaa, na kuwadhulumu. Na kufanya haki ni wajibu, lakini kufanya hisani pia ni jambo zuri linalopendekezwa. Na hilo ni kama vile kuwafaidi watu kwa mali, mwili, elimu, na aina nyinginezo za faida, hata kuwafanyia wema wanyama wanaoliwa na wengineo kunaingia humo. Na Mwenyezi Mungu alitaja kuwapa jamaa hasa, pamoja na kwamba wanaingia katika ujumla wa aya hii, ili kusisitiza haki yao na kukokoteza suala la kuwaunga, kuwafanyia wema, na kufanya bidii kubwa katika hilo. Na wanajumuishwa jamaa wote katika hilo, sawa wawe wa mbali wao au wa karibu wao, lakini kila mtu ambaye ni wa karibu zaidi, basi anastahili zaidi kufanyiwa wema. Na kauli yake, "na anakataza uchafu." Nao ni kila dhambi kubwa ambayo ni chafu kulingana na sheria na silika, kama vile ushirikina, kuua bila ya haki, uzinzi, wizi, kujiona, kiburi, kudharau viumbe na yasiyokuwa hayo miongoni mwa uchafu. Na inaingia katika maovu kila dhambi na uasi unaohusiana na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nayo dhuluma ni kila uvukaji mipaka kuhusiana na viumbe katika damu zao, mali zao, na heshima zao. Kwa hivyo, Aya hii imejumuisha maamrisho yote na makatazo yote, na hakikubakia chochote isipokuwa kinaingia ndani yake. Na vipengele vidogo vyote vinairudia kanuni hii, kwani kila jambo linalojumuisha uadilifu, au kufanya hisani, au kuwapa jamaa, basi hilo ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru. Na kila jambo ambalo linajumuisha uchafu, au uovu, au dhuluma, basi hilo ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alikataza. Na kwa hayo ndio unajulikana uzuri wa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru na ubaya wa yale ambayo alikataza. Na kwa hayo yanapaswa kupimwa maneno yote ya watu, na kuyarudishia hali zote. Basi ni mwingi wa baraka aliyeweka katika maneno yake uwongofu, uponyaji, nuru, kipambanuzi kati ya vitu vyote, na ndiyo sababu akasema, "Anawaaidhi" kwa yale aliyowabainishia katika kitabu chake, kwa maana amewaamrisha yale ambaye ndani yake kuna kutengenea kwenu kukubwa zaidi, na akawakataza yale ambayo ndani yake kuna madhara kwenu, "ili mpate kuyakumbuka" yale anayowaaidhi kwayo na mkayafahamu na kuyaelewa kwa hivyo mkatenda kwa mujibu wake, hivyo basi mkapata furaha ambayo hakuna huzuni wowote pamoja nayo.