Yusuf
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسْمَآءً سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَـٰنٍ ۚ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّآ إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ 40
{40} Na inavyojulikana ni kuwa yule ambaye hivyo ndivyo alivyo, na zilivyo sifa zake, ni bora zaidi kuliko miungu iliyo tofautitofauti, ambayo ni majina tu yasiyokuwa na ukamilifu wowote wala uwezo wa kutenda chochote. Na ndiyo maana akasema, "Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu." Yaani, mliwavalisha tu majina [na] mkawaita miungu, ilhali wao si chochote, wala hawana sifa yoyote ya uungu. "Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote." Bali Mwenyezi Mungu aliteremsha uthibitisho wa kukataza kuiabudu, na kubainisha ubatili wake. Na ikiwa Mwenyezi Mungu hakuiteremshia uthibitisho wowote, hawawezi hao kuwa ndio njia wala sababu wala ushahidi kwa hilo. Kwa sababu hukumu "ni ya mwenyezi Mungu" peke yake. Yeye ndiye Mwenye kuamrisha na kukataza, na kutunga sheria na kutunga hukumu mbalimbali, na Yeye ndiye aliyewaamrisha "msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka." Yaani, njia iliyonyooka inayofikisha kwenye kila heri. Na zisizokuwa hiyo miongoni mwa dini nyinginezo zote, hizo siyo nyoofu. Bali zilijipinda na zinafikisha kwenye kila uovu. "Lakini wengi wa watu hawajui" uhakika wa mambo. Vinginevyo, tofauti iliyopo kati ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika yeyote, na kumshirikisha ni jambo la dhahiri zaidi na bainifu zaidi kuliko mambo yote. Lakini kwa sababu ya kutokuwa na elimu kutoka kwa wengi wa watu juu ya hilo, yaliyotokea yale yaliyotokea ya ushirikina. Basi Yusuf, amani iwe juu yake, aliwalingania wale wafungwa wenzake wawili wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumfanyia yeye tu dini yao. Na inawezekana kwamba waliitikia na kufuata, basi neema ikatimia juu yao; na inawezekana kuwa hawakuacha kuwa katika ushirikina wao, kwa hilo hoja hiyo ikasimama juu yao.