Hud
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَـٰلِحًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَٱسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَٱسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓا۟ إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّى قَرِيبٌ مُّجِيبٌ 61
{61} Yaani: {Na" tuliwatuma "kwa Thamud." Nao ni kina 'Aadi wa pili, wanaojulikana, ambao walikuwa wakiishi huko Al-Hijr na Wadi Al-Qura, "ndugu yao" kwa nasaba, "Saleh" mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akiwalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Basi "Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu." Yaani, mpwekesheni yeye na mumfanyie yeye tu Dini. "Nyinyi hamna Mungu yeyote isipokuwa Yeye" si katika wakazi wa mbinguni wala katika wakazi wa ardhini. "Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika ardhi." Yaani, aliwaumba humo, na akasema: "Na akawaweka humo imara." Yaani, aliwafanya kuwa wafuatilizi humo na akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichikana, na akawaimarisha katika ardhi. Mnaweza kujenga, na kupanda, na kulima chochote mnachotaka, na mnafaidika kwa manufaa yake na kutumia masilahi yake. Kwa hivyo, kama vile hana mshirika yeyote katika hayo yote, basi msishirikishe na wengine katika kumwabudu. "Basi mwombeni msamaha" kwa yale mliyofanya ya kufuru, na ushirikina, na maasia na achaneni nayo, "kisha mtubu kwake." Yaani, rejeeni kwake kwa toba ya kweli na kurudi katika utiifu. "Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi." Yaani, yuko karibu na yule anayemwomba kwa dua ya kutaka kitu, au dua ya ibaada, naye humwitikia kwa kumpa ombi lake, na kuikubali ibada yake, na kumlipa kwayo malipo makubwa zaidi. Na jua kuwa ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni aina mbili: wa jumla na makhsusi. Basi ukaribu wa jumla ni ukaribu wake kwa elimu yake juu ya viumbe vyote ambao umetajwa katika kauli yake Mtukufu: "Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake." Na ukaribu mahususi ni Ukaribu wake kwa waja wake, wale wanaomuomba na wale wanaompenda. Nao ndio uliotajwa katika kauli yake Mtukufu: "Basi sujudu na ujongee!" Na katika Aya hii, na katika kauli yake: "Na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji." Na aina hii ya ukaribu inalazimu upole wake yeye Mtukufu na kuitikia kwake dua zao, na kutimiza kwake matashi yao. Na ndiyo maana jina lake "Al-Qarib (Aliye karibu)" huunganishwa na jina lake "Al-Mujib (mwenye kuitikia)."