Hud
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
فَلَعَلَّكَ تَارِكٌۢ بَعْضَ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيْكَ وَضَآئِقٌۢ بِهِۦ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَآءَ مَعَهُۥ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَآ أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ وَكِيلٌ 12
{12} Yeye Mtukufu anasema akimliwaza Mtume wake Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kukadhibisha kwa wakadhibishaji: "Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kikaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema, "Mbona hakuteremshiwa hazina." Yaani, hili halimfailii mfano wako, kwamba maneno yao yanakushawishi na yanakuzuia na yale uliyo juu yake, basi ukayaacha baadhi ya yale yanayoteremshwa kwako, na moyo wako ukaona dhiki kwa sababu ya ukaidi wao juu ya kusema kwao “Mbona hakuteremshiwa hazina, au Malaika akaja pamoja naye?" Kwa maana, maneno haya yanatokana na ukaidi, na udhalimu, usugu, na upotofu, na kutojua pahali pa hoja na ushahidi. Kwa hivyo, endelea na jambo lako wala zisikuzuie kauli dhaifu ambazo hazitoki isipokuwa kwa mpumbavu tu, wala kisione kifua chako dhiki juu yake. Kwani je, walikuletea hoja yoyote ambayo huwezi kuibatilisha? Au walitia doa baadhi ya yale uliyokuja nayo kwa doa ambalo linaathiri ndani yake na kupunguza hadhi yake ndiyo kikakubana kifua chako kwa sababu ya hilo? Au ni juu yako hesabu yao na kwamba unalazimika kuwaongoa kwa nguvu? "Hakika, wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa kila kitu." Basi Yeye ndiye mlinzi juu yao, na anayahifadhi matendo yao, na atawalipa ujira kamili zaidi.