Yunus
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَمَا كَانَ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ ٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ 37
{37} Yeye Mtukufu Anasema, “Na haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.” Yaani, haiwezekani wala haifikiriwi kwamba azuliwe Mwenyezi Mungu [Mtukufu] Qur-ani hii. Kwa sababu ni Kitabu Kikuu ambacho hakifikiwi na batili kwa mbele yake wala kwa nyuma yake, ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa zaidi. Nacho ni Kitabu ambacho lau kuwa wangekusanyika watu na majini ili walete mfano wake, basi hawangeleta mfano wake, hata kama wangesaidiana wao kwa wao. Nacho ni Kitabu ambacho alikizungumza kwacho Mola Mlezi wa walimwengu wote. Basi vipi ataweza binadamu yeyote kuzungumza kwa mfano wake au kitu cha karibu nacho ilhali maneno yanategemea ukuu wa mzungumzaji na sifa zake? Basi ikiwa yeyote anafanana na Mwenyezi Mungu katika ukuu wake na sifa za ukamilifu wake, angeweza kuleta mfano wa Qur-ani hii. Na hata kama tutajishusha tuyakubali uwezekano wa kuwepo hilo, na mtu akaizulia Mola Mlezi wa walimwengu wote, basi angemharakishia adhabu na akamfikishia mateso mara moja. Lakini Mwenyezi Mungu alikiteremsha Kitabu hiki kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, na ni hoja juu ya waja wake wote. Alikiteremsha “kisadikishe yale yaliyoitangulia” miongoni mwa vitabu vya mbinguni vya Mwenyezi Mungu, kwa namna ya kwamba kiliafikiana navyo na kikavisadikisha kwa yale vilivyoyashuhudia, na vikabashiria kuteremka kwake, na ikawa kama vilivyojulisha. "Na ni maelezo ya kina ya Kitabu” kuhusu yaliyo halali na ya haramu, na hukumu za kidini, na za kimajaliwa, na habari za ukweli “kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.” Yaani, hakina shaka yoyote ndani yake kwa namna yoyote ile. Bali ni haki ya yakini, ni uteremsho kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye alivilea viumbe vyote kwa neema zake. Na katika kubwa zaidi ya malezi yake ni kwamba aliwateremshia kitabu hiki, ambacho kina masilahi yao ya kidini na ya kidunia, na kinajumuisha tabia njema, na matendo mazuri.