Yunus
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَمَن يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ ٱلْمَيِّتَ مِنَ ٱلْحَىِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ 31
{31} Yaani, waambie hawa ambao walimshirikisha Mwenyezi Mungu na yale ambayo hakuyateremshia uthibitisho wowote, ukitoa hoja dhidi yao kwa yale waliyoyakiri ya kupwekeka kwa Mwenyezi Mungu katika umola wake, juu ya yale waliyoyakataa ya kupwekeka kwa Mwenyezi Mungu katika uungu. “Sema, "Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhi?” Kwa kuteremsha riziki kutoka mbinguni, na kutoa aina zake katika ardhi, na kurahisisha sababu zake humo. "Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona?” Yaani, ni nani aliyeviumba na ndiye mmiliki wake? Na alivitaja hivi hasa kwa sababu ni mbinu ya kukumbusha kilicho muhimu zaidi kwa kutaja kilicho chini yake, na kwa sababu ya ukamilifu wa cheo chake na manufaa yake. "Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti" kama vile kutoa aina mbalimbali za miti na mimea kutoka kwa mbegu na kokwa, na kumtoa Muumini kutoka kwa kafiri, na ndege kutoka kwenye yai... na mfano wa hayo? Na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai;” kinyume cha haya yaliyotajwa? “Na ni nani anayeyaendesha mambo yote" katika ulimwengu wa juu na wa chini? Na hili linajumuisha kila aina ya uendeshaji mambo wa kiungu. Kwa hivyo ukiwauliza kuhusu hayo, "Basi watasema, "Mwenyezi Mungu." Kwa sababu, wanayakiri hayo yote, na kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote katika kitu chochote miongoni mwa hayo yaliyotajwa. "Basi sema" uwaambie ukiwalazimisha kuikubali hoja hii, "Je, hammchi" Mwenyezi Mungu, na mkamuabudu Yeye tu, bila mshirika yeyote, na muwaache wale mnaowaabudu badala yake miongoni mwa wenza na masanamu?