Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 98 · Aya ya 8

Al-Bayyina 98:8

البينة

جَزَآؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِىَ رَبَّهُۥ

Maana

Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za mbinguni za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi. [8]

[8] Malipo yao Akhera kwa Imani na vitendo vyema walivyo vitanguliza, ni Mabustani ya kudumu yenye kupitiwa na mito kati yake, watakaa humo milele. Mwenyezi Mungu amepokea a'mali zao, na wao watamshukuru kwa hisani yake aliyo wafanyia. Hiyo ndiyo jaza ya mwenye kuiogopa adhabu ya Mola wake Mlezi, akaamini na akatenda mema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Malipo yao, mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama, ni Pepo ya makazi na utulivu, yenye upeo wa uzuri, ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito; watakaa milele humo. Allah Mtukufu Ameridhika nao, Akakubali amali zao njema. Na wao wameridhika naye kwa mapokezi Aliyowafanyia ya aina mbalimbali za takrima. Malipo mazuri hayo ni ya aliyemuogopa Mweyezi Mungu na akajiepusha na maasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Bayyina

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net