Al-Bayyina 98:4
البينةوَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ
Wala hawakufarikiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana. [4]
[4] Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu katika Mayahudi na Wakristo, ila baada ya kuwajia hiyo hoja iliyo wazi yenye kuonyesha ya kwamba Muhammad ndiye huyo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye ahidiwa katika Vitabu vyao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na manaswara, juu ya kuwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake walizokua wakiziona katika vitabu vyao, isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyeahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali, kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipopewa utume walimkanusha na wakatofautiana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net