Al-Alaq 96:19
العلقكَلَّا لَا تُطِعْهُ وَٱسْجُدْ وَٱقْتَرِب ۩
Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! [19]
[19] Kumnyamazisha huyu mwenye kuzuia, wewe usimkubalie kwa hayo anayo kukataza nayo, na dumu juu ya Swala zako, na endelea na sijida zako, na jijongeze kwa Mola wako Mlezi kwa hivyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mambo si kama Abû Jahl anavyoyadhania. Yeye, (ewe Mtume), hawezi kukufanya lolote la kukudhuru, Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu naye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net