Al-Alaq 96:15
العلقكَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًۢا بِٱلنَّاصِيَةِ
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! [15]
[15] Kwa kumkemea huyu mwenye kuzuia, anaambiwa kama hakuacha hayo anayo yafanya, basi hapana shaka tutamkokota kwa nguvu tukimshika kwa shungi lake la nywele mpaka Motoni!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mambo si kama anvyodai Abū Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika paji lake kwa nguvu na kumtia Motoni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net