Al-Balad 90:19
البلدوَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا هُمْ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ
Lakini waliozikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. [19]
[19] Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net