At-Tawba 9:2
التوبةفَسِيحُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ ۙ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُخْزِى ٱلْكَـٰفِرِينَ
Basi tembeeni katika ardhi miezi minne, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawahizi makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tembeeni katika nchi miezi mine, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anaye wahizi makafiri. [2]
[2] Basi nyinyi washirikina, mna amani kwa muda wa miezi mine, kuanzia tangazo hili, mzunguke mtakako katika muda huu. Lakini jueni kuwa popote mlipo nyinyi mko chini ya utawala wa Mwenyezi Mungu, na nyinyi hamuwezi kumshinda Yeye. Na mjue kuwa Mwenyezi Mungu amewaandikia hizaya iwapate hao wanao pinga.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tembeeni, enyi washirikina, katika ardhi muda wa miezi minne, mutembee mnapotaka mkiwa kwenye amani bila kusumbuliwa na Waumini, na mjue kwamba nyinyi hamtayaponyoka mateso. Na jueni kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuwatweza Makafiri na ni Mwenye kuwatia aibu hapa ulimwenguni na Moto kesho Akhera. Aya hii inawahusu wale waliokuwa na mapatano huru yasiyokuwa na muda au yule ambaye alikuwa kwenye makubaliano chini ya miezi minne, akamilishiwe miezi yake minne, au aliyekuwa na mapatano akayavunja.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net