Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 115

At-Tawba 9:115

التوبة

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوْمًۢا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapotosha kaumu baada ya kwishawaongoa mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwahisabu watu kuwa wamepotea baada ya kwisha waongoza mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. [115]

[115] Na si katika mwendo wa Mwenyezi Mungu na upole wake kwa waja wake kuwachukulia watu kuwa wamepotea, na awapitishie hukumu ya kuwatia khatiani na kuwapa adhabu, baada ya kwisha waongoza njia ya Uislamu, mpaka awabainishie kwa njia ya wahyi, ufunuo, kwa Mtume wake mambo ambayo inawapasa wajiepushe nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Hakuwa ni Mwenye kuwapoteza watu baada ya kuwapa neema, uongofu na taufiki, mpaka awaelezee waziwazi yale ambayo yatawapelekea kumcha Yeye na yale wanayoyahitajia ya misingi ya Dini na matawi yake. Hakika Allah Mtukufu, kwa kila jambo, ni Mjuzi; Amewafundisha nyinyi yale ambayo hamkuwa mkiyajua, amewaelezea waziwazi yale ambayo mtanufaika nayo na Amewasimamishia hoja kwa kuwafikishia ujumbe Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net