Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 87 · Aya ya 9

Al-A'laa 87:9

الأعلى

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ

Maana

Basi kumbusha, kama makumbusho yanafaa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. [9]

[9] Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi wakumbushe watu wako, (ewe Mtume), na uwaongoze njia yenye kheri nao, na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawaidha hayawaathiri isipokuwa yanawazidishia ujeuri na kuwafanya wayakimbie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'laa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net