Al-Burooj 85:8
البروجوَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa! [8]
[8] Na hapana walilo lichukia kwa hao Waumini ila ni kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu ambaye adhabu yake huogopwa, Msifiwa anaye tarajiwa thawabu zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Allah Mtukufu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake, Vitendo Vyake na sifa Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net