Al-Burooj 85:20
البروجوَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطٌۢ
Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. [20]
[20] Na Mwenyezi Mungu anawaweza hao, na anawajua vilivyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Amewazunguka kwa Ujuzi na uwezo Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qur’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net