Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 85 · Aya ya 11

Al-Burooj 85:11

البروج

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْكَبِيرُ

Maana

Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani za mbinguni zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [11]

[11] Hakika hao walio kusanya kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu vitendo vyema watapata Mabustani yapitayo mito kati yake. Neema hiyo waliyo lipwa ni kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari inapita mito, Huko ni kufaulu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Burooj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net