Al-Mutaffifin 83:14
المطففينكَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. [14]
[14] Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mambo yalivyo si kama wanavyodai! Bali hayo ni maneno ya Allah Mtukufu na Wahyi Wake kwa Mtume Wake. Na hakika zimezibwa nyoyo zao zikawa hazimkubali Allah Mtukufu, Na kile kilichoziziba nyoyo hizo ni kufunikwa na wingi wa madhambi wanayoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net