Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 78 · Aya ya 39

An-Naba 78:39

النبإ

ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا

Maana

Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anayetaka, na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi [39]

[39] Hiyo ndiyo siku isiyo na shaka. Basi atakaye na ashike njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi arejee kwa Imani, na a'mali njema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hiyo ndiyo siku ya haki isiyokuwa na shaka kuja kwake. Kwa hivyo, yule atakaye kuokoka na vitisho vya Siku hiyo, na ajifanyie njia ya marejeo kwa Mola wake kwa kutenda vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net