An-Naba 78:17
النبإإِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ كَانَ مِيقَـٰتًا
Hakika Siku ya uamuzi imewekewa wakati wake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, [17]
[17] Hakika siku ya uamuzi baina ya viumbe imewekewa miadi ilio kwisha kadiriwa kwa ajili ya kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe, nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalumu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net