Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 77 · Aya ya 38

Al-Mursalaat 77:38

المرسلات

هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَـٰكُمْ وَٱلْأَوَّلِينَ

Maana

Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. [38]

[38] Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hii ni Siku ambayo Allah Mtukufu Atatoa uamuzi baina ya viumbe, na ukweli na ubatilifu utabainika. Tutawakusanya nyinyi Siku hiyo, (enyi makafiri wa ummah huu), pamoja na makafiri wa mwanzo miongoni mwa ummah waliopita.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mursalaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net