Al-Insaan 76:21
الانسانعَـٰلِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوٓا۟ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavishwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. [21]
[21] Juu yao zipo nguo za hariri nyepesi za kijani, na nguo za hariri nzito. Na mapambo yao yaliomo mikononi mwao ni vikuku vya fedha. Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji kingine kilio safi, hakina uchafu wala najisi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Juu ya miili yao kuna nguo zilizoipamba, ambazo sehemu zake za ndani kuna hariri nyembamba ya rangi ya kijani, na nje yake kuna hariri nzito. Na miongoni mwa mapambo watakayovishwa ni vidani vya fedha. Na Mola wao Atawanywesha, katika sterehe hizo, kinywaji kisicho na uchafu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net