Al-Insaan 76:2
الانسانإِنَّا خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَـٰهُ سَمِيعًۢا بَصِيرًا
Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. [2]
[2] Hakika Sisi tumemuumba mwanaadamu naye ana sifa namna mbali mbali, kwa ajili ya kumtia mtihanini, majaribioni, baadaye. Kwa hivyo tukamjaalia awe anasikia na anaona, ili apate kuzisikia Aya na azione Ishara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tumemuumba binadamu kutokana na tone la manii la mchanganyiko wa maji ya mwanaume na maji ya mwanamke, ili tumtahini kwa kumuamrisha mambo ya kisheria baadaye, hivyo basi tumemfanya ni mwenye masikio ya kusikia na macho ya kuonea, apate kuzisikia aya na kuziona dalili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net