Al-Insaan 76:19
الانسانوَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا
Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasiopevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. [19]
[19] Na watakuwa wanawazunguka vijana ambao hawabadiliki hali yao, kwa furaha na sururi. Ukiwaona wanapo zunguka kwa wepesi na uchangamfu, utawadhania kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao, kama lulu zilizo tandazwa mbele yako zinang'ara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na watawazunguka wema hawa wavulana wenye hali moja ya kudumu wakiwatumikia, ukiwaona utawadhania, kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao na mng’aro wa nyuso zao, kuwa ni lulu iliyotenganishwa, inayong’ara.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net