Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 73 · Aya ya 7

Al-Muzzammil 73:7

المزمل

إِنَّ لَكَ فِى ٱلنَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا

Maana

Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani hakika mchana una shughuli nyingi. [7]

[7] Hakika mchana unakuwa na mambo mengi ya kukuhangaisha kutafuta maslaha ya maisha yako, na kushughulika na mambo ya kufikisha Ujumbe. Basi jiwekee nafsi yako faragha ya usiku kwa ajili ya kumuabudu Mola wako Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wewe katika kipindi cha mchana una wakati wa kuzunguka na kushughulika katika mambo yenye maslahi nawe, na kufanya harakati nyingi kwa majukumu ya utume, basi wakati wa usiku ipe nafasi nafsi yako kumuabudu Mola wako.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muzzammil

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net