Al-Jinn 72:18
الجنوَأَنَّ ٱلْمَسَـٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدًا
Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu. [18]
[18] Na imefunuliwa kwangu kwamba kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika misikiti ni ya kuabudiwa Allah Mtukufu Peke Yake, basi msiabudu humo asiyekuwa Yeye. Na mtakasieni maombi na ibada humo, kwani misikiti haikujengwa isipokuwa kwa ajili Allah Mtukufu Aabudiwe humo Peke Yake, na sio mwingine asiyekuwa Yeye. Katika aya hii kuna ulazima wa kuiepusha misikiti na kila kinachokoroga utakasaji wa Allah Mtukufu na ufuataji Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net