Al-Jinn 72:16
الجنوَأَلَّوِ ٱسْتَقَـٰمُوا۟ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَـٰهُم مَّآءً غَدَقًا
Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeliwanywesha maji kwa wingi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi, [16]
[16] Na hakika lau kuwa watu na majini wakifuata Njia ya Uislamu, wala wasende upogo wakaiwacha, basi bila ya shaka tutawanywesha maji mengi yatakayo enea nyakati za haja.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau makafiri wa kibinadamu na kijini wangefuata njia ya Uislamu na wasijiepushe nayo, tungewateremshia maji mengi, na tungewakunjulia riziki duniani,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net