Nooh 71:3
نوحأَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumtii.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii. [3]
[3] Ya kwamba mumt'ii Mwenyezi Mungu, na mumnyenyekee katika kutimiza waajibu zote; na mwogopeni Yeye kwa kuacha mnayo katazwa, na nit'iini mimi katika ninayo kunasihini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mimi ni mjumbe wa Allah Mtukufu kwenu. Muabuduni Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake na muogopeni Yeye, na nitiini katika kile ninachowaamrisha na kuwakataza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net