Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 71 · Aya ya 24

Nooh 71:24

نوح

وَقَدْ أَضَلُّوا۟ كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَـٰلًا

Maana

Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. [24]

[24] Na miungu hii iliwapoteza watu wengi. Na wala huwazidishii wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na inda, ili kuzidi kubaidika na Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wafuatwa wamewapoteza watu wengi kwa vile walivyowapambia njia za upotofu. Kisha Nûḥ akaendelea kusema, «Na usiwaongezee, ewe Mola wetu, hawa waliozidhulumu nafsi zao kwa ukanushaji na ushindani isipokuwa kuwaepusha na haki».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Nooh

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net