Al-Ma'aarij 70:32
المعارجوَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, [32]
[32] Na hao wenye kuzihifadhi amana za sharia na amana za waja wa Mwenyezi Mungu, na walio lazimika nayo kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu bila ya kukhuni wala kupunja,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale ambao wanazitunza amana za Allah Mtukufu na amana za waja, na wanatunza ahadi zao pamoja na ahadi za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, pamoja na za waja.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net