Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 70 · Aya ya 11

Al-Ma'aarij 70:11

المعارج

يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ ٱلْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِى مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍۭ بِبَنِيهِ

Maana

Ijapokuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, [11]

[11] Watakuwa wakijuulishana wao kwa wao mpaka wajuane baraabara, na ilhali hapana amuulizae mwenzie kitu. Kafiri atatamani lau ange pata kujikomboa nafsi yake na adhabu hiyo Siku ya Kiyama kwa kumtoa mwanawe awe ni fidia yake,

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watawaona na watawajua, na hakuna yoyote atakayeweza kumnufaisha yoyote. Kafiri atatamani kuikomboa nafsi yake na adhabu ya Siku ya Kiyama kwa watoto wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ma'aarij

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net