Al-Ma'aarij 70:1
المعارجسَأَلَ سَآئِلٌۢ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea! [1]
[1] Ameita, mwenye kuita, kuhimiza kama kufanya kejeli, iletwe upesi adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo hapana shaka itawashukia makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mmoja miongoni mwa washrikina amejiombea yeye na watu wake washukiwe na adhabu, adhabu ambayo ni yenye kuwapata siku ya kiama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net