Al-A'raaf 7:94
الأعرافوَمَآ أَرْسَلْنَا فِى قَرْيَةٍ مِّن نَّبِىٍّ إِلَّآ أَخَذْنَآ أَهْلَهَا بِٱلْبَأْسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ
Na hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote isipokuwa tuliwachukua wakazi wake kwa umaskini na maradhi ili wanyenyekee.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukumtuma Nabii yeyote katika mji ila tuliwapatiliza wakaazi wake kwa taabu na mashaka ili wapate kunyenyekea. [94]
[94] Na Sisi hatukumpeleka Nabii yeyote kwenye mji akawalingania watu wake wafuate Dini ya Mwenyezi Mungu iliyo sawa, na wao wakakataa kuukubali huo wito, ila tuliwapatiliza kwa ufakiri na maradhi, ili wapate kuwa wanyonge na wamwombe Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, na kumsafia niya wapate kuondokewa na balaa na wamuitikie Mtume wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukumtuma Nabii kwenye kijiji chochote kuwalingania watu wake kumuabudu Allah Mtukufu na kuwakataza ushirikina ambao wanao, kisha wakamkanusha, isipokuwa tuliwapa mtihani wa shida na mikasa, tukawatia kwenye miili yao magonjwa na ndwele, na katika mali yao ufukara na uhitaji, kwa matumaini kwamba wanyenyekee, waelekee kwa Allah Mtukufu na warudi kwenye haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net