Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 79

Al-A'raaf 7:79

الأعراف

فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَـٰقَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّى وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ ٱلنَّـٰصِحِينَ

Maana

Basi Swaleh akawaacha na akasema: Enyi watu wangu! Niliwafikishia Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikawanasihi, lakini nyinyi hamuwapendi wanaonasihi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi Swaleh akwaacha na akasema: Enyi watu wangu! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha. [79]

[79] Na kabla ya kuwateremkia adhabu hiyo ndugu yao Swaleh aliwaachilia mbali (kwa kukata tamaa nao), akawaambia: Enyi watu wangu! Mimi nimekufikishieni amri na makatazo ya Mola Mlezi wangu. Na nimekusafieni nasaha yangu, lakini nyinyi kwa ushindani wenu na ushupavu wenu, mmekuwa hamumpendi anaye kunasihini!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sãlih (amani imshukie), alijiepusha na watu wake, walipomchinja ngamia, na maangamivu yakawa ni yenye kuwashukia, na akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu! Nimewafikishia yale Mola wangu Aliyoniamuru niwafikishie, kuhusu maamrisho Yake na makatazo Yake, na nimewafanyia bidii kiasi nilichoweza katika kuwavutia kwenye kheri na kuwakemea shari na kuwa muaminifu, lakini nyinyi hamuwapendi waaminifu kwenu, ndipo mkayakataa maneno yao na mkamtii kila shetani aliyelaaniwa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net