Al-A'raaf 7:77
الأعراففَعَقَرُوا۟ ٱلنَّاقَةَ وَعَتَوْا۟ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا۟ يَـٰصَـٰلِحُ ٱئْتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Basi wakamuua yule ngamia, na wakaiasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakamuuwa yule ngamia, na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume. [77]
[77] Inda ya wenye kiburi ikakakamia, na wakampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamchinja Ngamia. Walivuka mpaka katika kiburi chao, wakaitupilia mbali amri ya Mola wao Mlezi, na wakasema kwa upinzani: Ewe Swaleh! Tuletee hiyo adhabu uliyo tuahidi ikiwa kweli wewe ni miongoni ya alio watuma Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakamchinja ngamia kwa kutojali onyo la Sãlih, na wakaingiwa na kiburi kilichowafanya wasifuate amri ya Mola wao na wakasema, kwa njia ya shere na kwa kuona kuwa adhabu iko mbali na wao, «Ewe Sãlih, tuletee hiyo adhabu ambayo unatuonya nayo, iwapo wewe ni miongoni mwa Mitume wa Allah Mtukufu!»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net