Al-A'raaf 7:74
الأعرافوَٱذْكُرُوٓا۟ إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ ٱلْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَٱذْكُرُوٓا۟ ءَالَآءَ ٱللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ
Na kumbukeni alivyowafanya wafuatizi (makhalifa) wa A’adi na akawaweka vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msienee katika nchi kwa kufanya uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kumbukeni alivyo kufanyeni wa kushika pahala pa A'adi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi. [74]
[74] Na kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu amekujaalieni ndio wa kurithi nchi ya A'ad, na akakupeni katika hiyo nchi makaazi mema, mkijenga majumba ya fakhari katika nyanda zake. Na mkichonga milima mkifanya majumba. Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, alivyo kuwekeni kwa makini katika nchi, wala msifanye maovu katika nchi, mkawa wenye kufisidi na kuharibu baada ya kukaa kwa makini kama huku.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni neema ya Allah Mtukufu juu yenu, Alipowafanya nyinyi mnashika nafasi za waliokuwa kabla yenu katika ardhi, baada ya kabila la ‘Ãd, Akawamakinisha nyinyi katika ardhi nzuri, mkaifanya makao, mkajenga kwenye mabonde yake majumba makubwa na mkayachonga majabali yake ili mfanye majumba mengine. Basi kumbukeni neema za Allah Mtukufu juu yenu na msizunguke katika ardhi kwa uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net