Al-A'raaf 7:72
الأعراففَأَنجَيْنَـٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا۟ مُؤْمِنِينَ
Basi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mizizi ya wale walio zikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini. [72]
[72] Basi Sisi tukamwokoa A'ad na walio amini pamoja naye kwa rehema yetu, na tukawateremshia makafiri cha kuwateketeza, na hapana chao kilicho bakia wala hapana athari yao, na wala hawakuingia katika kundi la Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi adhabu ya Allah Mtukufu ikatukia kwa kutumwa upepo mkali juu yao. Allah Mtukufu akamuokoa Hûd na walioamini pamoja na yeye kwa rehema kubwa kutoka kwake, Aliyetukuka. Na Akawaangamiza makafiri wote miongoni mwa watu wake, Akawavunjavunja mpaka wa mwisho wao. Na wao hawakuwa ni Waumini kwa kuwa walikusanya baina ya kukanusha aya za Allah Mtukufu na kuacha kufanya vitendo vyema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net