Al-A'raaf 7:70
الأعرافقَالُوٓا۟ أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ ٱللَّهَ وَحْدَهُۥ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Wakasema: Je, umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli. [70]
[70] Lakini wao juu ya wito mzuri huu walisema kwa kuona mageni: Hivyo wewe umetujia kututaka tumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja peke yake, na tuache masanamu waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Na hapana shaka sisi hatutofanya hayo, nawe tuletee hiyo adhabu unayo tutishia, kama wewe kweli ni katika wasema kweli!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
‛Ãd walisema kumwambia Hûd, amani imshukie, «Je, umetuita tumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, na tuihame ibada ya masanamu ambayo tumeirithi kutoka kwa mababa zetu? Basi tuletee adhabu ambayo unatutisha nayo iwapo wewe ni miongoni mwa wakweli katika hayo usemayo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net