Al-A'raaf 7:24
الأعرافقَالَ ٱهْبِطُوا۟ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَـٰعٌ إِلَىٰ حِينٍ
Akasema: Teremkeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Nanyi katika ardhi mtakuwa na makao na starehe mpaka ufike muda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda. [24]
[24] Mwenyezi Mungu akawaambia wao na pia na Shetani: Teremkeni nyote nyinyi, mtakuwa maadui nyinyi kwa nyinyi. Makao yenu na starehe yenu kwa muda mpaka ifike ajali yenu, yatakuwa katika ardhi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema, Aliyetukuka, kumwambia Ãdam, Hawwã’ na Iblisi, «Shukeni kutoka mbinguni muende ardhini, baadhi yenu mkiwa ni maadui wa wengine. Huko mtakuwa na mahala pa nyinyi kutulia na pa kujiliwaza mpaka muda wenu ukome».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net