Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 109

Al-A'raaf 7:109

الأعراف

قَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ عَلِيمٌ

Maana

Wakasema waheshimiwa kutoka katika kaumu ya Firauni, "Hakika huyu ni mchawi ajuaye vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi. [109]

[109] Musa alipo ionyesha Ishara ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, zilitibuka roho za wapambe wa Firauni na waheshimiwa wa kaumu yake, wakasema katika kujipendekeza kwa Firauni na kumtetea: Hakika huyu ni bingwa katika ilimu ya uchawi, wala hii si Ishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu!!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakubwa wa watu wa Fir‛awn walisema, «Hakika Mûsã ni mchawi, anayatawala macho ya watu kwa kuwadanganya mpaka ikawaingia kwenye fikira zao kuwa fimbo ni nyoka, na kukiona kitu kinyume na vile kilivyo, na yeye ana ujuzi mwingi wa uchawi na ana uhodari nao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net