Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 69 · Aya ya 9

Al-Haaqqa 69:9

الحاقة

وَجَآءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُۥ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتُ بِٱلْخَاطِئَةِ

Maana

Na Firauni na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta dhambi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. [9]

[9] Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na akaja mpita kiasi katika uasi, Fir’awn na ummah waliomtangulia waliokanusha Mitume wao, na wakazi wa vijiji vya watu wa Lûṭ ambao miji yao iligeuzwa chinijuu wakiwa ndani kwa sababu ya kitendo kibaya walichokifanya, cha ukafiri, ushirikina na mambo machafu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Haaqqa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net