Al-Qalam 68:4
القلموَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ
Na hakika wewe una tabia tukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika wewe una tabia tukufu. [4]
[4] Na hakika wewe bila ya shaka umeshikamana na sifa nzuri kabisa na vitendo vizuri kabisa alivyo kuumba navyo Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika wewe, (ewe Mtume), uko juu kwa tabia nzuri, nazo ni zile tabia njema zilizomo kwenye Qur’ani. Kwani kuifuata Qur’ani ilikua ni sifa yake, kwani alikua akitekeleza amri zake na kukomeka na yale yanayokatazwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net