Al-Qalam 68:32
القلمعَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ
Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. [32]
[32] Asaa Mola wetu Mlezi akatupa badala lilio bora kuliko hili shamba letu. Hakika sisi tunamtaka Mola wetu Mlezi peke yake atupe msamaha na malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tunatarajia kwa Mola wetu kuwa Atatupa kilicho bora zaidi kuliko shamba letu, kwa kuwa tumetubia na tumekubali makosa yetu. Sisi tuna matumaini mema kwa Mola wetu, tunatarajia msamaha na tunaomba kheri. Mfano wa mateso hayo tuliyowatesa nayo wenye shamba, ndivyo yanavyokuwa mateso yetu duniani kwa kila anayeenda kinyume na amri ya Allah Mtukufu, na akazifanyia uchoyo neema za Allah Mtukufu Alizompa, kwa kutotekeleza haki ya Allah Mtukufu katika neema hizo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net