Al-Mulk 67:3
الملكٱلَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِى خَلْقِ ٱلرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ ۖ فَٱرْجِعِ ٱلْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ
Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudia kutazama! Je, unaona kosa lolote?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote? [3]
[3] Yeye ndiye aliye zizua mbingu saba zilizo pandana kwa mpango mmoja sawa sawa. Huoni tafauti yoyote katika uundaji wa Mwenyezi Mungu, ambaye rehema yake imeenea kwenye viumbe vyake vyote. Basi hebu tazama tena, unaona khitilafu yoyote?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Aliyeumba mbingu saba zilizopangika, baadhi yake juu ya nyingine, huoni katika uumbaji wa Allah Mtukufu (Mwingi wa rehema), ewe mwenye kuangalia, tofauti yoyote, basi rudia tena kuangalia mbinguni: je unaona mpasuko wowote au nyufa?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net