Al-Mulk 67:13
الملكوَأَسِرُّوا۟ قَوْلَكُمْ أَوِ ٱجْهَرُوا۟ بِهِۦٓ ۖ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Na ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi; hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ficheni kauli zenu, au zitangazeni; hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. [13]
[13] Na ficheni kauli yenu, au itangazeni. Yote mawili kwa Mwenyezi Mungu ni sawa, kwani Yeye ni Mkuu wa kuyazunguka yote kwa kuyajua, Mjuzi wa vinavyo ficha vifua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yaficheni maneno yenu, (enyi watu), katika jambo lolote miongoni mwa mambo yenu, au yadhihirisheni, kwani yote mawili mbele ya Allah Mtukufu ni sawa. Hakika Yeye, kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi wa yaliyomo ndani ya vifua, yatafichika vipi maneno yenu na matendo yenu Kwake?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net