At-Taghaabun 64:14
التغابنيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ مِنْ أَزْوَٰجِكُمْ وَأَوْلَـٰدِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَٱحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا۟ وَتَصْفَحُوا۟ وَتَغْفِرُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. [14]
[14] Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu, ambao wanakuzuilieni msimt'ii Mwenyezi Mungu kwa kutaka kuwatimizia hao matakwa yao. Basi kuweni na hadhari nao. Na mkiweza kuyavuka makosa yao yanayo kubalika kusameheka, na mkayapuuza, na mkawafichia, basi Mwenyezi Mungu naye atakughufirieni nyinyi. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira na rehema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake! Kwa hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui wenu, wanawazuia na njia ya Allah Mtukufu na wanawavunja moyo katika kumtii Allah Mtukufu, basi jihadharini nao wala msiwasikilize. Na iwapo mtayasamehe makosa yao, mkayapa mgongo na mkayaficha msiyatangaze, basi Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe na ni Mwingi wa rehema, Atawasamehe madhambi yenu, kwani Yeye, Aliyetakasika na kila upungufu, ni Mkubwa wa kusamehe na ni Mkunjufu wa rehema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net