Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 61 · Aya ya 13

As-Saff 61:13

الصف

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini! [13]

[13] Na neema nyengine ambazo Waumini Mujahidina wanazo zipenda, ni msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu utakao kuleteeni kheri zake. Na ewe Muhammad! Wabashirie Waumini kuwa watapata malipo haya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kuna neema nyingine kwenu, (enyi Waumini), mtaipenda, nayo ni msaada kutoka kwa Allah Mtukufu utakaowajia na ushindi wa haraka mtakaoupata kwa mikono yenu. Na wape bishara Waumini, (ewe Mtume), ya kunusuriwa na kupata ushindi duniani na kupata Pepo kesho Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saff

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net