Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 60 · Aya ya 1

Al-Mumtahana 60:1

الممتحنة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ عَدُوِّى وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَآءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا۟ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلْحَقِّ يُخْرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَـٰدًا فِى سَبِيلِى وَٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِى ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعْلَمُ بِمَآ أَخْفَيْتُمْ وَمَآ أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyokujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu, basi ameipotea njia ya sawa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi ameipotea njia ya sawa. [1]

[1] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Msiwafanye maadui wangu na maadui wenu kuwa ni wenzenu mkiwapa mapenzi ya kweli, na hali wao wameyakataa yaliyo kujieni nyinyi ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu chake. Wamemtoa Mtume na wamekutoeni nyinyi kwenu kwenye majumba yenu, kwa sababu ya Imani yenu kumuamini Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Mnapotoka makwenu kwenda pigana Jihadi katika Njia yangu na kutaka radhi yangu, basi msifanye urafiki na adui zangu, mkawapa mapenzi kisirisiri. Na Mimi nayajua vyema yote mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na yeyote mwenye kumfanya adui wa Mwenyezi Mungu kuwa ndiye rafiki yake basi ameikosea Njia Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini (Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo)! Msiwachukue maadui wangu na maadui wenu mkawafanya ni marafiki halisi na vipenzi, mkawa mnaamiliana nao kwa upendo na mkawapasha habari za Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Waislamu wengine, na hali wao wameikanusha haki iliyowajia ya kumuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na Qur’ani iliyoteremshwa kwake. Wanamtoa Mtume na wanawatoa nyinyi, (enyi Waumini), kutoka Makkah kwa kuwa nyinyi mnamuamini Allah Mtukufu Mola wenu na mnampwekesha. Mkiwa nyinyi, (enyi Waumini), mmehama katika hali ya jihadi katika njia yangu kwa kutafuta radhi yangu kwenu, basi msifanye urafiki na maadui wangu na maadui wenu. Mnawaambia kwa siri kuwa mnawapenda, na mimi ninayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha. Na yoyote anayefanya hivyo miongoni mwenu, ashakosea njia ya haki na usawa na amepotea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mumtahana

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net